Mtunzi: Paschal Florian Mwarabu
> Tazama Nyimbo nyingine za Paschal Florian Mwarabu
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 2,980 | Umetazamwa mara 7,311
Download NotaEnyi Watumishi wa Bwana
Enyi watumishi wa Bwana sifuni
Lisifuni lisifuni Jina la Bwana
Na ahimidiwe Bwana Mungu
Bwana Mungu kutoka Sayuni
Akaaye Yerusalemu aleluya
1. Ninyi msimamao nyumbani mwa Bwana
Nyuani mwa nyumba ya Mungu wenu
Msifuni Bwana kwa kuwa yu mwema
Liimbieni jina lake kwa maana lapendeza
2. Kwa sababu Bwana amejichagulia Yakobo
Na Israeli wawe watu wake hasa
Maana najua mimi ya kuwa Bwana ni mkuu
Na Mungu wetu yu juu ya miungu yote
3. Enyi mlango wa Israeli mhimidini
Enyi mlango wa Haruni mhimidini
Enyi mlango wa Lawi mhimidini Bwana
Enyi mnaomcha Bwana mhimidini Bwana