Mtunzi: Ronaldo Nakaka
> Mfahamu Zaidi Ronaldo Nakaka
> Tazama Nyimbo nyingine za Ronaldo Nakaka
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani | Ekaristi / Komunio | Tenzi za Kiswahili
Umepakiwa na: Ronald Nakaka
Umepakuliwa mara 2,153 | Umetazamwa mara 6,471
Download Nota Download Midi1. Nakupenda Yesu mokozi wangu na Bwana wangu sina mwingine katika mbingu hata duniani wewe peke uzima wangu hata nikiwa jaribuni na shida nyingi zimenisonga moyoni mwangu ninatambua mtetezi wangu yu ngali hai
2. Nina fahamu kukupenda wewe nikumpenda jirani kwanza adui zangu kuwaombea kuwasamehe wakinikosea kuwapa nguo wasio nazo hata chakula wasionacho wagonjwa nao kuwaombea hata wafungwa kuwatembelea
3. Neema yako nategemea huruma yako yanihuisha mjono wako unanilinda na jina lako limeniokoa Ee Yesu mfalme unisikie usinipite siku ya leo ufanye jambo moyoni mwangu maishani mwangu uniuishe
4. Msalabani ametufia na dhambi zetu amezitwaa kwa damu yake yenye thamani ametukomboa dhidi ya shetani umkaribishe moyoni mwako akawe Bwana na mokozi wako abadilishe mwenendo wako maisha yako ayabariki