Ingia / Jisajili

Usiogope

Mtunzi: Ronaldo Nakaka
> Mfahamu Zaidi Ronaldo Nakaka
> Tazama Nyimbo nyingine za Ronaldo Nakaka

Makundi Nyimbo: Tenzi za Kiswahili

Umepakiwa na: Vusile Silonda

Umepakuliwa mara 485 | Umetazamwa mara 2,020

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Utavuka jangawni kwenye ukame mkuu
    Bila kufa kwa kiu
    Utatembe nyikani na kufika salama
    Ingawa hujui njia
    Utauona uso wa Mungu nawe utaishi.
 
Kiitikio
 
Usiogope kwani daima nakutangulia
Usifadhaike moyoni daima nakuangalia
Njoo, njoo kwangu usiogope
Njoo, nitakupa pumziko.
 
2. Utavuka bahari, yenye mawimbi makali
Bila kugharikishwa
Utapita kwenye moto, wenye miali hatari
Bila kuteketea
Utauona uso wa Mungu nawe utaishi.
 
 
3. Utasema na watu, mataifa mageni
Nao wataelewa
Wote wa watajua, Mimi ni Mungu wa kweli
Nami nitatukuzwa
Utauona uso wa Mungu nawe utaishi.
 
 
4. Ungalionja mauti, kamba za kuzimu
Jua nipo nawe,
Japo ungalikufa, wewe ungaliishi
Kwani waniamini
Utauona uso wa Mungu nawe utaishi.

Maoni - Toa Maoni

Emmanuel LIBAKU Feb 06, 2019
Asante sana ndugu Ronald kwa nota za mziki huu. naomba unisaidie na nota za mziki BE NOT AFRAID. nimeutafuta sija pata.

Toa Maoni yako hapa