Mtunzi: Fr. Aloyce Msigwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Fr. Aloyce Msigwa
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 5,505 | Umetazamwa mara 11,098
Download Nota Download MidiNatamani kujongea kwenye altare yako ili nami nishiriki kwenye karamu ya Bwana Yesu x2
Ni uone uzuri wa Bwana uliomo katika fumbo takatifu la Ekaristi mwili na damu ya Yesu
Nimpokee Bwana Yesu Kristu na kuishi pamoja nae siku zote akae ndani yangu nami ndani yake
1. Bwana naomba unijalie moyo wa uchaji nitubu dhambi nami nijongee meza yako
Ninakuomba unijalie usafi wa moyo nikupokee nikiwa katika hali njema
2. Karamu yako ni takatifu tena ya amani iliyojaa upendo na uzima milele
Na wale watakao shiriki kwenye meza imewapasa kujua vema siri yako
3. Uwajalie huruma yako na mapendo yako uwatie nguvu wote wasio kupokea
Kwa nguvu yako uwainue walioanguka waondoe vizuizi vinavyo waangusha
4. Uwaalike wanao wote kwenye meza yako waishiriki karamu ya uzima wa milele
Wafurahie amani yako na mapendo yako yaliyofichwa kwenye fumbo hili takatifu