Mtunzi: Faustine J. Mtegeta
> Tazama Nyimbo nyingine za Faustine J. Mtegeta
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 23,030 | Umetazamwa mara 32,468
Download Nota Download MidiLeteni ndama walionona madhabahuni kwa Bwana tena toeni bila kinyongo moyoni ndipo mtabarikiwa naye x 2
1. Leteni ndama aliyeshiba majani ya kondeni, mkamtolee Mungu Baba yenu kwa shukrani.
2. Peleka sadaka yako iliyo safi na ya kupendeza, ndipo utakapokitikisa kiti cha mwenyezi.
3. Kumbuka yule mjane aliyetoa senti moja, alibarikiwa na kuongezewa na mwenyezi.
4. Sadaka iliyo safi ni ile inayokugusa wewe, hiyo ndiyo sadaka iliyo safi sana.
5. Isaka alitolewa na baba yake kama sadaka, hivyo Abrahamu alizidishiwa uzao wake.