Mtunzi: Erick Nyaga (Prince)
> Mfahamu Zaidi Erick Nyaga (Prince)
> Tazama Nyimbo nyingine za Erick Nyaga (Prince)
Makundi Nyimbo: Noeli
Umepakiwa na: Erick Nyaga (Prince)
Umepakuliwa mara 61 | Umetazamwa mara 66
Download Nota Download Midi1.Malaika akamtokea,Bikira Maria Mwenye heri,akampasha habari kuwa,atampata mtoto Yesu.
(Ni Noeli) Ni Noeli leo ni furaha,(mkombozi) mkombozi Yesu kazaliwa.
(Alleluia) Alleluia heri ya Noeli,(ni Noeli) ni Noeli na tumsuyudu.
2.Mamajusi toka mashariki,waongozwa na mwanga wa nyota wasafiri hadi Bethlehemu,kusudi kumsuyudu Yesu.
3.Walipofika Bethlehem,wakaenda walipoongozwa,wakamkuta mtoto Yesu,amelazwa horini mwa ng'ombe.
4.Nao wakamtolea zawadi,dhahabu ubani na manemane,wakamwabudu na kumsuyudu,kweli wamezaliwa mfalme.