Ingia / Jisajili

Ni Shangwe Jubilei Ya Mapadri (Miaka 100)

Mtunzi: Robert A. Maneno (Aka Albert)
> Mfahamu Zaidi Robert A. Maneno (Aka Albert)
> Tazama Nyimbo nyingine za Robert A. Maneno (Aka Albert)

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito

Umepakiwa na: Albert Maneno

Umepakuliwa mara 634 | Umetazamwa mara 3,242

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

NI SHANGWE JUBILEI (YA UPADRI), NI MWAKA WA MAPADRI; MIAKA MIA MOJA (YA UPADRI), KANISA TANZANIA.

WAUMINI WAKATOLIKI TANZANIA TWAFURAHI, MIAKA MIA MOJA IMETIMU YA UPADRI WA WAZAWA;

BABA MUNGU TWASHUKURU (ASANTE), UTUME WA UPADRI, UMEIMARIKA SANA, KATIKA KARNE HII MOJA; TWAWAOMBEA BARAKA (MAPADRI), UWAJALIE NEEMA, WATUNZE KIAPO CHAO, KAMA WALIVYOTAMANI

MASHAIRI

1.     KANISA LIMEJENGWA JUU YA PETRO,”WEWE NDIWE PETRO, NA JUU YA MWAMBA HUU; NITALIJENGA KANISA; WALA MILANGO YA KUZIMU, HAITALISHINDA”.

2.     “NENDENI DUNIANI KOTE MKA-HUBIRI INJILI”, NI AGIZO LAKE BWANA; “YULE AAMINIYE, AAMINIYE NA KUBATIZWA, ATAOKOKA.

3.     ”PADRI KI-MSINGI NI MUHUDUMU WA NENO LA MUNGU, SAKRAMENTI ZA KANISA; KWA NAMNA YA PEKEE, EKARISTI TAKATIFU, NA KITUBIO”.

4.       PADRI MWIRABURE, PADRI KIPANDA, PADRI MUPAPI, NA PADRI KYAKARABA; MAPADRI WAZALENDO, ZAO LA KWANZA LA MAPADRI, WATANZANIA.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa