Maneno ya wimbo
Niacheni niacheni Mimi niende (niende)//niacheni nikatangaze neno lake ,pande zote kuu za dunia wote walisikie, waliishi maishani mwao uzima wajipatie , Ni a che ni,(niacheni )..niacheni nikalihubiri neno lake lipate kuenea.
1.Niache niende kutangaza neno lake ,kwa mataifa yote kwa mataifa yote watu wote duniani wakusifu wewe.
2.Njooni wazee njooni pia vijana / njooni watoto wote / mapadrepia watawa makasisi wote waje wakusifu wewe.
3.Niache niende kulihubiri neno kwa masikini wote / kwa matajiri wote walemavu na wajane wakufate wewe.
Na mwisho Ee Mungu sifa na kurudishia (Mungu wangu )/ kinanda filimbi na ngoma kayamba vipigwe..
Soprano / niacheni niimbe ,niacheni nicheze ,niacheni niruke Mimi nimsifu Mungu ,nimwimbie Mungu.
Alto/ Mimi niimbe Mimi acheni nicheze Mimi niruke nimsifu Mungu nimwimbie Mungu.
Tenor/ acheni niimbe acheni nicheze,acheni Mimi niruke nimsifu Mungu nimwimbie Mungu.
Bass//Niacheni mi niimbe pigeni na ngoma nicheze,niacheni mi niruke Mimi niruke nimsifu Mungu nimwimbie Mungu.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu