Mtunzi: Davis Charles Ungele
> Mfahamu Zaidi Davis Charles Ungele
> Tazama Nyimbo nyingine za Davis Charles Ungele
Makundi Nyimbo: Miito
Umepakiwa na: Davis Charles Ungele
Umepakuliwa mara 1 | Umetazamwa mara 0
Download Nota Download MidiNimeamua mwenyewe Mimi kumtumikia Mungu wangu nami nimeitikia wito wako nikutumikie wewe.
Bila msaada wako Mungu Mimi siwezi lolote Bwana hivyo nishike mkono Bwana wangu nifike mwisho salama.
1. Nitume popote Bwana nikaieneze injili watu wakakutambue wewe walishike neno lako.
2. Niende hospitalini niwahudumie wagonjwa watambue kuwa wewe Yesu ndiye mponyaji wao.
3.Nikawe mwalimu shuleni niwafundishe wanafunzi na wao wajue ya kwamba ni wewe mwalimu wao.
4.Sauti yangu ikusifu Kwa nyimbo na tenzi za sifa ili wewe Bwana Mungu wangu uhimidiwe milele.
5.Nitume vitani Bwana nikawaokoe mateka waone ya kuwa wewe Bwana ni Mfalme wa amani.