Mtunzi: Joseph Rimisho
> Mfahamu Zaidi Joseph Rimisho
> Tazama Nyimbo nyingine za Joseph Rimisho
Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio
Umepakiwa na: JOSEPH RIMISHO
Umepakuliwa mara 1,279 | Umetazamwa mara 3,247
Download Nota Download MidiShairi
1.Nimeionja Ekaristi, karamu ya uzima mpya.
Hakika Kristo yuko hai, ameshibisha roho yangu.
Kiitikio
(Yesu mpenzi wa roho yangu nakutamani we, Yesu mpenzi wa roho yangu nipokee leo).x2
Mashairi
2.Yesu amenipa uhai, roho yangu yafurahia.
Kwani yeye ndiye mpaji, na mlishi wa roho zetu.
3.Nimetubu na dhambi zangu, ili nimpokee Yesu.
Yesu akiwa ndani yangu, hunifariji moyo wangu.
4.Hima ndugu jongea mbele, ushiriki karamu hii.
Uyafute makosa yako, uyaache na ya dunia.