Ingia / Jisajili

Nimekuja kukushukuru

Mtunzi: Patrick Lutego
> Mfahamu Zaidi Patrick Lutego
> Tazama Nyimbo nyingine za Patrick Lutego

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Patrick Lutego

Umepakuliwa mara 435 | Umetazamwa mara 1,471

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Nmewaza nakufikiri mema uliyo nitendea, yote niliyonayo ni we umenijalia, Nimekuja kukushukuru we we ulie nguvu zangu, nitakase moyoni nifanyike chombo chako, Ee Bwana pokea sifa nakusifu moyoni mwangu, in wewe uliniumba, kwa kusudi nikutumikie. ..2) Machafuko yalipovuma yakatikisa chombo changu, nilipofika mwisho mwishoni mwa kufikiri, Nilijua nimepoteza nimepoteza Neema yako, kumbe upo chomboni mawimbi kuyatuliza, Ee Bwana......3)Mara nyingi uliniita nikashupaza moyo wangu, kwakuzigeukia sauti zidanganyazo, hali yangu ilipokua mfano wa vazi chakavu, lakini wewe Bwana hukuyatazama hayo, Ee Bwana....4) Niwapo hekaluni mwako uzikumbuke sala zangu, kwani moyoni mwangu nakiri uweza wako, utazame shauku yangu yakukupenda siku zote, ningali ni dhaifu Bwana unihurumie, Ee Bwana........

Nyimbo nyingine za mtunzi huyu

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa