Ingia / Jisajili

Ninakuabudu Mungu Wangu (Adoro Te Devote)

Mtunzi: Traditional
> Tazama Nyimbo nyingine za Traditional

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Alex Rwelamira

Umepakuliwa mara 815 | Umetazamwa mara 1,231

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
1. Ninakuabudu Mungu wangu, unayejificha altareni, ninakutolea moyo wangu, usiofahamu siri yako

2. Mafahamu yangu yadanganya, yanapokuona na kugusa, namsadiki Yesu hadanganyi, yeye Mungu Mwana na ukweli

3. Waficha Umungu msalabani, na ubinadamu altareni, nami naungama zote mbili, kama mwivi yule mwenye toba

4. Tomas aligusa majeraha, nami nasadiki bila shaka, ewe Yesu nipe pendo lako, tumaini kwako na imani

5. Umeteswa nini Bwana mwema, kwa kunipa mkate wa uzima, Yesu unifiche ndani yako, ili nilionje pendo lako

6. Yesu Pelikane nitazame, na kwa damu yako nitakase, tone moja ndilo linatosha, na dunia yote yaokoka

7. Ndani ya mafumbo Yesu yumo, atafumbuliwa kwangu lini, nikuone Yesu uso wako, nishiriki nawe heri yako

Amina!

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa