Ingia / Jisajili

Niruhusu Ee Yesu Nijongee

Mtunzi: Elias Fidelis Kidaluso
> Tazama Nyimbo nyingine za Elias Fidelis Kidaluso

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 30,267 | Umetazamwa mara 49,694

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Ni ruhusu Yesu wangu niijongee meza yako unisamehe dhambi Mwokozi uje Rohoni mwangu uniokoe njoo kaa ndani yangu nami nikae ndani yako ili nipate amani tele ndani ya Roho yangu nifarijike

Wewe Bwana wanijua wanijua hata nafsini mwangu wewe ndiwe tabibu pekee war oho yangu tena ndiwe kimbilio langu x2

1.       Tazama Yesu wangu ninajongea karamu yako

Pengine kwako Bwana sikustahili kuijongea

Unihurumie Ee Yesu wangu unisamehe

2.       Hakika kwako Bwana makosa mengi nimeyatenda

Ubinadamu wangu siwezi kuficha kwako Bwana

Unihurumie Ee Yesu wangu unisamehe

3.       Niwazi Yesu wangu unaujua udhaifu wangu

Sina chakujitolea mbele yako Ee Yesu wangu

                      Unihurumie Ee Yesu wangu unisamehe


Maoni - Toa Maoni

mwesigawillibardmsg@gmail.com Dec 20, 2022
Naomba namba zako za simu mtunzi wa wimbo huu

Kahindi Misigah Jul 09, 2021
Kia kweli huu Wimbledon wapendeza sana. Hongera mtunzi.

CONSTANT WANJALA Feb 06, 2020
napenda dana utunzi wenu, Mungu azidi kuwabariki

Amos Renatus May 09, 2018
Hongera Sana E. Kidaluso kwa Wimbo mzuri

Duncan Ndakalu Mar 09, 2018
naomba nyimbo zako nyingine,heko sana kwa ujumbe wa wimbo huu ambao unaniguza sana

Novart Gwoma Jan 01, 2018
hongera sana mtunzi, maneno na ujumbe wote unanifariji sana napo usikia huu wimbo. Barikiwa sana kwa utunzi wako mpendwa katika Bwana

James Sengo Gabriel Jan 16, 2017
Natoa pongezi kwa mtunzi wa wimbo huu, mungu azidi kumbariki sana ktk kazi yake, naipenda sana kazi hii

mary kafyome Jan 01, 2017
Hongera sana wimbo huu unamtafakarisha mtu kabla ya kuijongea meza ya bwana hongeara sana mtunzi

nikolaus shabate Dec 18, 2016
tumaini letu.....?ndg zangu wakristu tumtegemee mungu kwa kila jambo 0782791709\0767418456

nicolaus peter shabate Dec 18, 2016
tumaini letu ............?ndg zangu wakristu tumtegemee mungu kwa kila jambo

nicolaus shabate Dec 18, 2016
hongera sana mtunzi wa wimbo huu

Nicolaus shabate Dec 18, 2016
Wimbo huu inatufundisha kuwa tujiandae tuandae roho zetu tusitende dhambi tujiweke tayari mbele za mungu ,pia nakumbukia ubatizo wangu june .29.2001 jimbo kuu la mbulu _manyara

nikolaus Dec 18, 2016
nampongeza mtunzi wa wimbo huu ,tuendelee na utume wetu

paschal Oct 26, 2016
Mimi nimeupenda naomba mnisaidie audio yake au video yake naipataje

Mushy Jul 27, 2016
Hengera sana

ERNEST MAGUNUS Jul 13, 2016
wimbo mzuri sana tuendelee na utume.

Toa Maoni yako hapa