Ingia / Jisajili

Nitakaa Nyumbani Mwa Bwana

Mtunzi: Eng.Richard Samson
> Mfahamu Zaidi Eng.Richard Samson
> Tazama Nyimbo nyingine za Eng.Richard Samson

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Zaburi

Umepakiwa na: Shiivah Ric

Umepakuliwa mara 0 | Umetazamwa mara 0

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 28 Mwaka A

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana, nyumbani mwa Bwana milele x2.

1. Bwana ndiye mchungaji wangu, mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu,

Katika malisho ya majani mabichi hunilaza, kando ya maji ya utulivu huniongoza.

2. Hunihuisha nafsi yangu, huniongoza katika njia za haki kwa ajili ya jina lake.

Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, Sitaogopa mabaya.

3. Waandaa meza, meza  mbele yangu, machoni pa watesi wangu.

Umenipaka mafuta kichwani pangu, na kikombe changu kinafurika.

4. Hakika wema na fadhili zitanifuata, siku zote za maisha yangu;

Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele, nyumbani mwa Bwana milele.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa