Mtunzi: Gervas M. Kombo
> Mfahamu Zaidi Gervas M. Kombo
> Tazama Nyimbo nyingine za Gervas M. Kombo
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Gervas Kombo
Umepakuliwa mara 840 | Umetazamwa mara 2,957
Download Nota Download MidiNITAKUSIFU EE MUNGU - By: G.M.Kombo
Nitakusifu ee Mungu kwa moyo wangu wote, nitatangaza habari za matendo yako ya ajabu, nitafurahi na kushangilia kwa sababu yako nitaimba sifa zako ee Mungu mkuu x2
1. Maana adui zangu wamerudi nyuma, wameanguka na kuangamia ulipowakabili
2. mataifa wamezama katika shimo walilolifanya kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao
3. umenitetea bwana nakunipa haki yangu, umekaa katika kiti cha enzi na kuhukumu kwa haki
4. kwa maana mhifadhi hatasahauliwa daima, matumaini ya wanyonge hayatapotea milele