Ingia / Jisajili

Nitamwimbia Bwana

Mtunzi: Michael Shija
> Mfahamu Zaidi Michael Shija
> Tazama Nyimbo nyingine za Michael Shija

Makundi Nyimbo: Pasaka

Umepakiwa na: Michael Shija

Umepakuliwa mara 1,734 | Umetazamwa mara 4,987

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Nitamwimbia Bwana kwamaana ametukuka sana, kwamaana ametukuka amaetukuka sana x2

01.Farasi na mpanda farasi amewatupa Baharini,                               

Bwana ni nguvu zangu na wimbo wangu,

Naye amekua wokovu wangu,

Yeye ni Mungu wangu name nitamsifu,

Ni Mungu wa baba yangu name nitamtukuza.

02. Bwana ni mtu wavita Bwana ndilo jina lake,

Magari ya Farao na jeshi lake amewatupa bahari ya Shamu

vilindi vimewafunikiza wamezama vilindini kama jiwe

03. Bwana mkono wako wakuume umepata fahari ya uweza,

Bwana mkono wako wa kuume wawasetaseta adui,

Kwa wingi wa ukuu wako wawaangusha chini wanaokuondokea.

04. Utawaingiza na kuwapanda katika mlima wa urithi wako,

Mahali pale ulipojifanyia Ee Bwana ili upakae,

Pale patakatifu ulipopaweka imara Bwana kwamikono yako,

Bwana atatawala milele na milele.


Maoni - Toa Maoni

Geoffrey Jan 23, 2020
Napongeza

Toa Maoni yako hapa