Mtunzi: Filbert Munywambele (Fimu)
> Tazama Nyimbo nyingine za Filbert Munywambele (Fimu)
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Basil Tumaini
Umepakuliwa mara 931 | Umetazamwa mara 4,216
Download Nota Download MidiSALA NI NINI
Na. Filbert Munywambele
Kiitikio:
Sala ni nini ndugu yangu? Hebu nieleze.
Sala nimazungumzo na Mungu wetu x 2
kuinua moyo na akili kwake na kuyatafakari matendo yake kwetu. X 2
Tusali pamoja katika familia, tusali pamoja katika jumuia/
Tuombe amani katika nchi yetu, tuombe amani katika bara letu.
Mashairi:
1. Sala ni mahusiano yakinifu na Mungu, inahitaji umakini, uaminifu, usikivu kati yako na Mungu wako.
2. Sala ni kuonesha hisia zetu, kufungua moyo wetu na akili zetu kwa Mungu.
3. Sala ni kujiweka mbele ya Mungu, mkutano wa upendo Mungu na binadamu
4. Sala ni kumwendea aliye juu: Utatu mtakatifu, Mungu mmoja.