Mtunzi: Eradius Kanyaruju
> Tazama Nyimbo nyingine za Eradius Kanyaruju
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Anthem
Umepakiwa na: Eradius Kanyaruju
Umepakuliwa mara 815 | Umetazamwa mara 5,046
Download Nota Download Midi1.) Shule yetu I beshi tazama yapendeza, kwa mazingira yake majengo na usafi. Imejengwa kando ya kilima na barabara pia hali nzuri ya hewa yavutia. Yapatikana mkoani Mwanza, wilaya ilemela kata ya nyakato. Kumbukeni kumbukeni elimu ni nuru, wanafunzi na walimu twambua. Wazazi na walezi niwajibu wenu kuwapatia elimu watoto wenu.
2.) Shule yetu Ibeshi sote twaipenda, inayo madarasa nadawati za kutosha. Waalimu wenye juhudi kwenye kazi yao wanafunzi wenye nidhamu ndani na nje. Kwenye taaluma pia na michezo, usafi wa mwili pia mazingira. Kumbukeni kumbukeni elimu ni nuru wanafunzi na walimu twatambua, Wazazi na walezi niwajibu wenu kuwapatia elimu watoto wenu.
3.) Karibuni watu wote hapa shuleni kwetu, Wazazi na walezi tuungane pamoja. Tudumishe mshikamanoo kwa nguvu zote umoja ni nguvu utengano udhaifu. Wageni wote pia wahisani tunawahitaji pia twawapenda. Kumbukeni kumbukeni elimu ni nuru, wanafunzi na walimu twatambua. Wazazi na walezi ni wajibu wenu kuwapatia elimu watoto wenu.