Maneno ya wimbo
Kiitikio : Tazama mtumishi wako nakuja mbele yako Bwana, naitikia wito wako Ee Bwana nitume mimi ×2
Nami nitakwenda Ee Bwana kwa mataifa yote, niwahubirie maskini habari njema×2
1. Wewe Bwana wanijua, mimi ni mdhaifu, nakuomba unitakase, na kwa watu wako niende.
2. Roho wako nijalie, yeye aniongoze na nielewe neno lako, na kwa watu wako niende.
3. Nijalie ushupavu, nihubiri Imani, tena bila ya kuogopa, na kwa watu wako niende
4. Bwana undiminished, kwenye utume wangu, niweze kuishi upendo, na kwa watu wako niende.
5. Bwana unisaidie, nisitamani mali, kwa nguvu niwatumikie, na kwa watu wako niende.