Maneno ya wimbo
TUNAKUSHUKURU.
Tunakushukuru Mpaji wa vyote, Ee Bwana Yesu asante, kwa mema yako uliyotujalia, twakuomba ukae nasi , (ulinde roho zetu x 2), na upokee shukrani zetu twaomba (na upokee shukrani zetu pokea x 2)
Mashairi
1. Upendo wako kweli ni wa ajabu, umetulisha mwili wako na kutunywesha damu yako, Asante Ee Bwana Yesu kwa karamu uliyotujalia.
2. Upendo wako kweli ni wa ajabu, Ee Bwana Yesu umetujalia uzima wa mwili na roho, moyo wangu unajaa furaha siku zote.
3. Upendo wako kweli ni wa ajabu, ulisema aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu, hukaa ndani yangu nami hukaa ndani yake.
4. Upendo wako kweli ni wa ajabu, umetujalia neema ya Karamu ya chakula cha mbinguni wote tuliompokea, tumezipata neema zake.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu