Ingia / Jisajili

Tung'ang'anie

Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 2,068 | Umetazamwa mara 5,020

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

Wapenzi tung'ang'anie imani yetu tushikilie imani yetu tusiachie imani yetu tushikilie Imani yetu haya haya
(Imani ya babu zetu imani yetu ya Baba zetu) x 2

  1. Tujifunze kwa babu Abrahamu Abrahamu aliyeahidiwa mtoto uzeeni, akaamini Abrahamu akapata, akaamini babu yule na akapata.

  2. Abrahamu kaahidiwa uzao uzao tele kama mchanga baharini na nyota mbinguni, akaamini Abrahamu akapata, tena taifa teule Israeli.

  3. Abrahamu kaambiwa amchinje kwa mkono wake mwanawe wa pekee Isaka bila kosa, kanyenyekea Abrahamu katukuzwa, hata leo babu yule ametukuka

Hitimisho

Oho Hima hima wapenzi tuing'ang'anie imani urithi namba moja tuing'ang'anie imani daraja tegemeo tuing'ang'anie imani la kwenda uwinguni tuing'ang'anie imani hima hima wapenzi tuing'ang'anie imani.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa