Ingia / Jisajili

Tuwe Na Huruma

Mtunzi: Nestory C. Madaso
> Mfahamu Zaidi Nestory C. Madaso
> Tazama Nyimbo nyingine za Nestory C. Madaso

Makundi Nyimbo: Mwaka wa Huruma ya Mungu

Umepakiwa na: Alfonce Haule

Umepakuliwa mara 295 | Umetazamwa mara 1,443

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO:

Tuwe na huruma (ndugu), tuwe na msamaha, kwa watu wote, kama Baba yetu wambinguni, alivyonahuruma. X 2

Tuwasamehe wenzetu, makosa waliyotukosea, kama Baba yetu wambinguni anavyotusamehe X2.

1. Tuwahudumie Wagonjwa, bila ya kuwabagua, kama Baba yetu wambinguni, anavyotutendea sisi.

2.Tuwahudumie Wajane, Yatima nao Wazee, kama Baba yetu wambinguni, anavyotutendea sisi.

3.Tuwahudumie Vipofu, Viwete na Walemavu, kama Baba yetu wambinguni, anavyotutendea sisi.

4. Tuwahudumie Wafungwa, nao wenye matatizo, kama Baba yetu wambinguni, anavyotutendea sisi.


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa