Mtunzi: Massawe. A. F.
> Tazama Nyimbo nyingine za Massawe. A. F.
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Antusa Felix
Umepakuliwa mara 774 | Umetazamwa mara 1,961
Download Nota Download Midi//Twendeni wote na vipaji ((II&IV:vyetu) tukavitoe (I&III: altareni) (II&IV:kwake Bwana); Mungu wetu tumshukuru mema (II&IV:mengi) katujalia// x2.
1. (a) Twendeni na fedha za mifuko yetu; tukampe Bwana ni mali yake.
(b) Alitupa kusudi tumtolee; twendeni kwake sasa tukasitoe.
2. (a) Twendeni na mazao ya mashambani; tukampe Bwana ni mali yake.
(b) Kwa baraka ya mvua yalisitawi; twendeni kwake sasa tukayatoe.
3. (a) Twendeni na sala za mioyo yetu; tuzitoe madhabahuni pake.
(b) Na kwa huruma zake atasikia; na kutujalia tunayoomba.
4. (a) Twendeni na dhabihu za kushukuru; tumshukuru Mungu muumba wetu.
(b) Tumwombe tena baraka na neema; za kuweza kumtumikia yeye.