Ingia / Jisajili

Uje Roho Mtakatifu

Mtunzi: S. E. Mlugu
> Tazama Nyimbo nyingine za S. E. Mlugu

Makundi Nyimbo: Pentekoste

Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela

Umepakuliwa mara 6,895 | Umetazamwa mara 31,787

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Shangilio Pentekoste

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
 1. Uje Roho Mtakatifu tuangaze toka mbingu, Roho zetu kwa mwangao, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 2. Uje Baba wa maskini, uje mtoa wa vipaji, uje mwanga wa mioyo, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 3. Ee Mfariji mwema sana, ee rafiki mwanana, ee raha mustarehe, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 4. Kwenye kazi u pumziko, kwenye joto burudisho, u mfutaji wa machozi, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 5. Ewe mwanga wenye heri, uwajaze waamini, neema yako mioyoni, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 6. Bila nguvu yako wewe, mwanadamu hana kitu, kwake yote yana kosa, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 7. Osha machafuko yetu, panyeshee pakavu petu, na kuponya majeraha, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 8. Ulegeze ukaidi, pasha moto ubaridi, nyoosha upotevuu wetu, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 9. Wape waamini wako, wenye tumaini kwako, paji zako zote saba, Ewe Mungu Roho njoo.
   
 10. Wape tuzo ya fadhila, wape mwisho bila ila, wape heri ya milele, Ewe Mungu Roho njoo.

Maoni - Toa Maoni

Charles Fungilwa Jun 01, 2019
Kristu! Nabarikiwa sana ninapousikia ukiimbwa huu wimbo, najisikia ndo nashukiwa na Ndimi za Moto za Roho Mtakatifu. Ahsante mtunzi S. E Mlugu ubalikiwe sana

Catherine kessy May 13, 2019
Huwa nabarikiwa sana sana sana niusikiapo ukiimbwa ,naupenda mno,hongera kwa mtunzi,kutoka moyoni naupenda

Joachim Kawishe Nov 22, 2018
Wimbo huu ni hazina kubwa ya kwani kila niuimbapo Roho mtakatofu amashuka na nguvu zake.

Gerald Ernest Ndanzi0767 Sep 13, 2018
Napongeza sana kwa wimbo mzuri nashauri kabla ya kufanya jambo lolote tumwite kwanza Roho mtakatifu atatuongoza katika kweli

JOACKIM MBAULE Jun 11, 2018
Wimbo kiukweli ni mzuri ila siwezi nikapinga

Angela Chizziel May 03, 2018
Hongera sana kwa kufanya Wakristo Wakatoliki kupata Nyimbo hii katika mitandao. Mungu awabariki sana.

Valerian Modaha Feb 12, 2018
Nawapongeza mno kwa nyimbo nzuri za kugusa na kuamsha mioyo iliyolala

Japhet Jan 31, 2018
Nafurahi sana kwa nyimbo nzuri mungu awazidishie MAISHA

anuary patern Sep 01, 2017
Nimebarikiwa sanaaa

Premji Kiwale Aug 08, 2017
Mungu Atuzidishie Iman Yetu Milele Na Milele.

Fred Charles Apr 30, 2017
Mungu na atubariki sote

jastin Mar 15, 2017
mungu awabariki

Anneth Epimack Nov 29, 2016
Kutoka moyoni nawapongeza, nimebarikiwa

faustina Nov 11, 2016
Bataka za mungu na ziwe juu yako.

Paulo haule Oct 20, 2016
Pongezi kwako mpedwa mungu akubaliki

Steven maduhu Jul 08, 2016
Utukufu wa MUNGU upo ndani ya wimbo huo

Toa Maoni yako hapa