Mtunzi: S. E. Mlugu
> Tazama Nyimbo nyingine za S. E. Mlugu
Makundi Nyimbo: Shukrani
Umepakiwa na: Martin Munywoki
Umepakuliwa mara 2,879 | Umetazamwa mara 5,322
Download Nota Download MidiKwa kinywa changu Mungu wangu nitakutukuza,
kwa nyimbo nzuri nitaziimba sifa (zako )
Kwa kuwa Mungu wema wako kwangu mimi ni mkuu siwezi kuelezea
{ Sina kitu Bwana cha kukupa (wewe)
kulingana na mema uloyatenda
Naitoa kwako nafsi yangu (Bwana)
nitendee unavyotaka } *2
1. Kama ni pumzi ya uhai umenipa bure,
Sauti nzuri ya kuimbia, yatoka kwako
Nakurudishia sifa na shukrani
2. Kama ni elimu, niliyo nayo ni mali yako,
Ujuzi na kazi niliyo nayo vyatoka kwako
Nakurudishia sifa na shukrani
3. Magonjwa mengi umeniponya ee Mungu wangu,
Na ajali nyingi umenikinga ee Mungu wangu
Nakurudishia sifa na shukrani