Mtunzi: Kelvin Masoud
> Mfahamu Zaidi Kelvin Masoud
> Tazama Nyimbo nyingine za Kelvin Masoud
Makundi Nyimbo: Kwaresma
Umepakiwa na: kelvin masoud
Umepakuliwa mara 265 | Umetazamwa mara 1,783
Download Nota Download MidiShairi 1..Ninalia kwa uchungu ewe Yesu wangu,mateso makali uliyoyapata maumivu makali uliyapata Bwana,
Kiitikio..Uliteseka Ee Yesu wangu mpaka kufa pale msalabani,(sauti ya 1)kwa uchungu ulisema,(wote)....Baba kikombe hiki kinihepuke, nisipokinywa,nisipokinywa,mapenzi yako yatimize .
Shairi 2..Majonzi yalinipata niliposhudia,msalaba mzito ulioubeba ulianguka chini kwa uchungu mkubwa.
Shairi 3..Misumari ulichomwa bila huruma, madonda makubwa mwili damu tupu uliteseka sana na uliwasamehe.
Shairi 4.Hukupaswa kuteseka ewe Yesu wangu,kwa kutukomboa ulimwaga damu ju ya msalaba Bwana ulikata roho.