Ingia / Jisajili

UMEBATIZWA NA UNATUMWA

Mtunzi: Gabriel D. Ng'honoli
> Mfahamu Zaidi Gabriel D. Ng'honoli
> Tazama Nyimbo nyingine za Gabriel D. Ng'honoli

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Miito | Ubatizo

Umepakiwa na: Gabriel D. Ng'honoli

Umepakuliwa mara 1,513 | Umetazamwa mara 2,858

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
KWAYA YA YESU KRISTO MFALME PAROKIA YA KATUBUKA (Ujumbe wa Mwezi pekee wa Kimisionari 2019) UMEBATIZWA NA UNATUMWA Maneno & na Muziki: G.D.Ng’honoli KIITIKIO Ewe Mkristo uliyebatizwa ukaikiri Imani yako Katoliki kwa ubatizo, Mama kanisa anakutuma nenda Katangaze Injili; anakutuma kutangaza Injili kaitangaze Injili kwa Mataifa. Mama Kanisa anakutuma nenda kakemee maovu, Watu watubu dhambi wamrudie Mungu, washiriki Ekaristi na Sakramenti nyingine za Kanisa. MAIMBILIZI 1. Umebatizwa na kufanywa kuhani wa Kristo kaihubiri injili katika familia na katika Jumuiya ndogo ndogo za Kikristo ipelekwe shuleni, kwa wanafunzi wa dini na palipo watu wengi ili Injili ilete Amani kwa watu. 2. Kuhubiri injili ni jukumu la kila mbatizwa tuhubiri Imani kwa maneno na matendo; tuwasaidie yatima, wajane na wagonjwa, tuwape matumaini waliokata tamaa. Tuwasaidie wafungwa na walemavu, tuwatetee wale wasio na sauti wasikike, tuondoe maisha ya hofu na vitisho, hiyo ndiyo kazi yetu wabatizwa, kumpeleka Kristo kwa watu wote. 3. Utume wa Yesu baada ya ubatizo ni umisionari tosha twapaswa kuuiga kama wabatizwa, kwa kufuata nyayo za Kristo katika kuhubiri Imani yetu na kueneza Ufalme wa Mbinguni kwa watu wote.

Maoni - Toa Maoni

Petro Aug 22, 2024
Hongereni sana kwa kazi nzuri ya kuinjilisha kupitia app hii. Naomba msaada wa wimbo HAKIKA BWANA HUJANIACHA mtunzi ni Gabriel G.Ng'honoli

Toa Maoni yako hapa