Ingia / Jisajili

Uturehemu ee Bwana

Mtunzi: Erick Kessy
> Mfahamu Zaidi Erick Kessy
> Tazama Nyimbo nyingine za Erick Kessy

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Zaburi

Umepakiwa na: ERICK KESSY

Umepakuliwa mara 261 | Umetazamwa mara 402

Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Jumatano ya Majivu
- Katikati Dominika ya 1 ya Kwaresma Mwaka A

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

(K) Uturehemu ee Bwana, kwakuwa tumetenda dhambi.

1.Ee Mungu unirehemu,

   sawawawa na fadhili zako/

   kiasi cha wingi wa rehema zako,

   uyafute makosa yangu,

   unioshe kabisa na uovu wangu,

   unitakase dhambi zangu.

2.Maana nimejua mimi makosa yangu,

   na dhambi yangu i mbele yangu daima/

   nimekutenda dhambi wewe peke yako,

   na kufanya maovu mbele za macho yako.

3.Ee Mungu uniumbie moyo safi,

   uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu/

   usinitenge na uso wako,

   wala roho yako Mtakatifu usiniondolee.

4.Unirudishie furaha ya wokovu wako,

   unitegemeze kwa roho ya wepesi/

   Ee Bwana uifumbue midomo yangu,

   na kinywa changu kitazinena sifa zako. 


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa