Ingia / Jisajili

Viumbe Nyi Vya Dunia

Mtunzi: Traditional
> Tazama Nyimbo nyingine za Traditional

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Anophrine desdeus

Umepakuliwa mara 7 | Umetazamwa mara 8

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
VIUMBE NYI VYA DUNIA
(Misale Ndogo Na. 231; Tuimbe Pamoja Na. 84)
1. Viumbe nyi vya dunia/ Na vya mbingu njoni,
Sogeeni kuangalia/ Hapa kuna nini!
Ndiyo Kuu Sakramenti/ Ni Yesu wa Ekaristi,
Twende mwabudia/ Chini ya Hostia.
2. Wa Malaika Malkia/ Njoo shuka kwetu,
Mwabudia mwangukia/ Mwanao Mungu Mtu,
Ututie shime Mama/ Tuweze mpenda daima,
Leo duniani/ Kesho uwinguni.
3. Enyi pia Malaika/ Wakazi wa juu,
Jongeeni kwa furaha/ Kuimbia Mkate huu,
Mitume na manabii/ Mabikira, Mashahidi,
Nanyi Karibuni/ Yesu mtukuzeni.
4. Twende nasi masikini/ Mwangukia Yesu,
Ni mpenzi wetu amini/ Mlo wa roho zetu,
Kwake heri hapa chini/ Kwake raha uwinguni,
Asifiwe pote/ Na viumbe vyote.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa