Mtunzi: S. D. Masanja
> Tazama Nyimbo nyingine za S. D. Masanja
Makundi Nyimbo: Sadaka / Matoleo
Umepakiwa na: Ludovick Michael
Umepakuliwa mara 1,779 | Umetazamwa mara 5,204
Download Nota Download Midi(Sasa ni wakati mzuri wa kwenda mbele zake Bwana, twendeni kwa Bwana Mungu, tukatoe sadaka) *2
(tukatoe sadaka kwake Bwana Mungu mwenyezi naye ataipokea, kuitakasa na kuibariki, kuigeuza (iwe) mwili na damu ya Bwana Yesu mwokozi wetu na mkombozi wetu) *2
MASHAIRI
1. Tazama Bwana tunakuja kwako tukiwa na furaha tele, tunaleta sadaka yetu, tunaleta sadaka yetu ni kazi ya mikono yetu tumepata vyote kwa wema wako Bwana, pokea.
2. Tazama Bwana tunakutolea sadaka yetu leo Bwana, kwa unyenyekevu wa moyo, twaomba upokee Bwana, kazi ya mikono uliyotujalia, pokea
3. Ee Mungu baba muumba wa mbingu wewe ni mungu wetu milele, haufananishwi na yeyote, wema wako hauna mipaka, hauna kipimo wewe ni mungu wetu milele.