Mtunzi: Paschal Florian Mwarabu
> Tazama Nyimbo nyingine za Paschal Florian Mwarabu
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari | Shukrani
Umepakiwa na: Thomas George Mwakimata
Umepakuliwa mara 2,312 | Umetazamwa mara 4,928
Download Nota Download MidiWakristu tusali Rozari Tuombe Amani Kwetu Tanzania x 2:
1. Vita na shida vinatishia dunia, mateso mengi yanasonga ulimwengu.
2. Njaa magonjwa, yameenea mahali pengi, watoto wetu wanateseka siku zote.
3. Nchi nyingi ziko katika machafuko, chuki na hila, zimeikumba dunia.
4. Akina mama wanahangaika na watoto, wanateseka, nchini mwao wenyewe.
5. Mapigano, mabomu yanawaua wengi, amani kweli, amani imeshapotea.
6. Tumsifu Mama, atuombee kwake Mungu, atuepushe, na madhara hayo makubwa.