Mtunzi: A. K. C. Sing'ombe
> Tazama Nyimbo nyingine za A. K. C. Sing'ombe
Makundi Nyimbo: Juma Kuu | Kwaresma
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 9,026 | Umetazamwa mara 15,052
Download Nota Download MidiSING'OMBE
AKC 25/02/1994
Yesu wangu niokoe
ulimwegu nilimo ni mateso nishike mkono wangu Bwana niokoe
Ulikuja duniani kwa wadhambi nitakase kwa damuyo Bwana nitakate
Bwana nakukimbilia
1. Nionyeshe uso wako uso mkunjufu nisamehe dhambi nakusihi mwokozi Bwana unisikie
2. Nimefanana na mwana mwana mpotevu dhiki na karaha vimenisonga sana Bwana unisikie
3. Wewe ndiwe ngome yangu ngao yangu tumaini langu ninakutegemea Bwana unisikie
4. Roho yangu mwili wangu vyote ni vyako ndivyo ulivyoumba viimarishe Bwana, Bwana unisikie
5. Mungu Baba Mungu mwamba Mungu mkombozi Mungu wa mapaji Utatu mtakatifu Usifiwe milele