Ingia / Jisajili

Faraja Ya Kweli

Mtunzi: Gerald R. Mussa
> Mfahamu Zaidi Gerald R. Mussa
> Tazama Nyimbo nyingine za Gerald R. Mussa

Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari

Umepakiwa na: Gerald Mussa

Umepakuliwa mara 498 | Umetazamwa mara 1,729

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO:

Sasa mimi niende wapi(mimi)(mimi) Bwana wangu(Yesu),yani tabu ni nyingi Bwana ndugu wamekibilia mbali,mimi(Sauti ya IV.Bwana wangu ninakulilia wewe naomba amani yako Bwana) nalia,nalilia faraja faraja ya kweli inatoka kwako Bwana.x2

  1. Nanyenyekea kwako nalia mbele yako,maadui ni wengi Bwana wangu wanaoitamani roho yangu,unilinde Bwana wangu niokoe.
  2. Kila kukicha Bwana kwangu ni masengenyo,wananisingizia ya uongo wanazifurahia tabu zangu,wewe Bwana umebaki nguvu yangu.
  3. Kwangu hapakaliki dhiki na matatizo,nimekuwa mkiwa duniani sasa wanidhihaki nakusema, yuko wapi Bwana wako tumuone.
  4. Kwako kuna furaha, kwako kuna amani pia kuna mapendo na neema,nipo kati ya waovu na wadhambi,niepushe niokoe kati yao.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa