Mtunzi: Bernard Mukasa
> Mfahamu Zaidi Bernard Mukasa
> Tazama Nyimbo nyingine za Bernard Mukasa
Makundi Nyimbo: Mafundisho / Tafakari
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 13,977 | Umetazamwa mara 28,767
Download Nota Download MidiMwenyezi ameniumba akanileta kati yenu niwakumbushe watu wake thamani yenu duniani x2
Acheni kufa moyo acheni kukata tama yeye aliyewaumba anaijua kazi yakex2
1. Aliijua siri yenu hata kabla hamjaumbwa ramani ya maisha yenu yote imo mikononi mwake
2. Magonjwa yanayo watesa na maumivu yasiyo koani madogo kuliko yale aliyoyaponya kwa sekunde
3. Hali mbaya ya kiuchumi mlo mmoja madeni mengi ni njia ya kunyenyekeana kumpa Mungu utukufu
4. Misiba inayowaliza mnapofiwa na ndugu zenu ni njia ya wapendwa wenu kwenda mbinguni wakafurahi
5. Maumivu yakuonewa kudhulumiwa kusingiziwa ni njia ya wapendwa wenu kwenda mbinguni wakafurahi
6. Matatizo ya ndoa zenu na migogoro ya familia ni bahati mmejaliwa ya kujifunza uvumilivu
7. Nadhili ngumu za utawa, misukosuko ya ukasisi ni kuuvua ulimwengu na kulivaa koti la uwingu
8. Bebeni misalaba yenu nyamazeni msinung’unike huo ndio wokovu wenu shikilieni msiachie