Mtunzi: B N Mogeni
> Mfahamu Zaidi B N Mogeni
Makundi Nyimbo: Pasaka
Umepakiwa na: Brian Mogeni
Umepakuliwa mara 3 | Umetazamwa mara 10
Download Nota Download Midi
AMEFUFUKA MWOKOZI
Sop & Alto: Jumapili (Mapema) asubuhi kaburi (la Yesu liko) li wazi, jiwe limevingirishwa kando kaburini hayumo x2. (Yu wapi) Amefufuka Bwana ameenda Garilaya twende Garilaya tushuhudie. Amefufuka Bwana amefufuka Mwokozi, Mkombozi wetu aleluya.
Tenor & Bass: Mapema asubuhi kaburi (la Yesu liko) li wazi, jiwe limevingirishwa kando kaburini hayumo x2. (Yu wapi) Amefufuka Bwana ameenda Garilaya tuandamane Kwenda Garilaya tushuhudie. Amefufuka Bwana amefufuka Mwokozi, amefufuka mkombozi wetu aleluya.
1. Maria Magdalena,Maria mama wa Yakobo naye Salome walilikuta kaburi likiwa wazi na mwili haupo.
2. Malaika kawaambia, msiogope najua mnamtafuta yesu aliyekufa hayupo hapa amefufuka.
3. Yesu kawaambia, msiogopee nendeni mkawaambie ndugu zangu waende Garilaya huko wataniona.
4. Aleluya tuimbe sasa, vigelegele tupige tumshangilieamefufuka leo, kashinda kifo yu mzima tena.