Mtunzi: Noel S.Munyetti
> Mfahamu Zaidi Noel S.Munyetti
> Tazama Nyimbo nyingine za Noel S.Munyetti
Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mafundisho / Tafakari | Majilio
Umepakiwa na: Noel Seni Munyetti
Umepakuliwa mara 17 | Umetazamwa mara 23
Download Nota Download Midi1. Nimetenda uovu mwingi na kufanya kinyume nawe. Nimekuwa mdhambi mimi, sistahili rehema zako. Nimeiharibu nafsi yangu.
(K) Nimesimama mbele yako, ninakiri makosa yangu.
( Maisha yangu yameniweka mbali, mbali nao uso wako Mungu wa wokovu wangu unirehemu ) ×2
2. Maisha yangu yasikitisha, mambo yangu nifanyayo yamenitenga na Mungu wangu. Sina nilichoweka Mbinguni.
3. Muumba wangu nimemuasi, nimeshindwa kuilinda na kuijali Imani yangu. Dhambi I juu yangu daima.
HITIMISHO:
(Mungu wangu Bwana wangu, unisamehe dhambi zangu.
Ninakiri dhambi zangu, naomba Bwana nirehemu )