Ingia / Jisajili

Baba Asante Sana

Mtunzi: Alphonce Andrew Otieno Obonyo
> Mfahamu Zaidi Alphonce Andrew Otieno Obonyo
> Tazama Nyimbo nyingine za Alphonce Andrew Otieno Obonyo

Makundi Nyimbo: Shukrani

Umepakiwa na: Alphonce Andrew Otieno Obonyo

Umepakuliwa mara 14 | Umetazamwa mara 24

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

BABA ASANTE SANA

Alphonce OBONYO

KIITIKIO

Baba ,Asante sana, asante baba Baba, asante sana.

Kwa wema wako,  baba asante sana. Asante sana , asante, Baba asante sana.


BETI YA 1

A

Kwa pumzi ya uhai uliyonipa,
Kwa jua lichomozalo kila siku,
Kwa mikono yako inayonilinda,
Baba Mungu wangu, nakushukuru.

B

Unanipa siku, unanipa nguvu,
Unanisitiri katika mapendo,
Hata ninapokuwa dhaifu njiani,
Mkono wako haukuniacha.


BETI YA 2

A

Kwa meza yako unayotu alika,
Kwa mwili wa Kristu, mkate wa uzima,
Kwa damu yo Kristu watunga nisha,
Baba Mungu wangu, nakushukuru.

B

Twapokea Kristo,
Twapokea nguvu,
Mwili wa Kristo tunaungana,
Baba Mungu wangu, nakushukuru.



BETI YA 3

A

Kwa familia unayonijalia,
Kwa ndugu zangu wanaonizunguka,
Kwa upendo wako watuunganisha,
Baba Mungu wangu, nakushukuru.

B

Unanipa ndugu hata marafiki,
Unatufunika kwa upendo wako,
Hata tunapokuwa dhaifu njiani,
Hutulinda kwa pendo.


BETI YA 4

A

Kwa Neno lako linaloniongoza,
Kwa nuru yako inayonimulika,
Kwa Roho wako unatuongoza,
Baba Mungu wangu, nakushukuru.

B

Unanipa hekima,
Unanipa nuru,
Unaniongoza njia zako njema,
Hata ninapokuwa gizani njiani,
Neno lako liniongoza. 


Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa