Ingia / Jisajili

BWANA AMEJAA HURUMA NA NEEMA

Mtunzi: Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Mfahamu Zaidi Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Pascal Mussa Mwenyipanzi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Pascal Mussa

Umepakuliwa mara 336 | Umetazamwa mara 848

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
BWANA AMEJAA HURUMA NA NEEMA Kiit: Bwana amejaa, Bwana amejaa, Bwana amejaa huruma na neema, si mwepesi wa hasira ni mwingi wa fadhili, si mwepesi wa hasira ni mwingi wa fadhili. 1.Ee nafsi yangu umhimidi Bwana wangu, naam vyote vilivyo ndani yangu mimi, vilisifu jina lake takatifu, wala usisahau wema wakee, Umsifu Bwana wako siku zote. 2.Ndiye anakusamehe dhambi zako zote, hata na magonjwa yeye akuponya, na uhai wako anaukomboa, na uhai wako anaukomboa, akomboa kwenye kifo na mauti. 3.Tena Bwana wetu akutia taji, taji la fadhili na rehema zake, kweli yeye hatateta siku zote, kweli yeye hatateta siku zote, milele hasira yake hatashika. 4.Na hatuadhibu vile tunavyostahili, kadiri ya dhambi zetu halipizi, mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, wema wake ni mkuu kwa wamchao. 5.Kama vile mashariki ipo mbali ipo mbali mbali nayo magharibi, ndivyo alivyo ziweka dhambi zetu, ndivyo alivyo ziweka dhambi zetu, alivyoziweka mbali mbali nasi.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa