Ingia / Jisajili

EE BWANA UWE PAMOJA NAMI KATIKA TAABU ZANGU Zab 91

Mtunzi: Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Mfahamu Zaidi Pascal Mussa Mwenyipanzi
> Tazama Nyimbo nyingine za Pascal Mussa Mwenyipanzi

Makundi Nyimbo: Kwaresma | Mazishi | Zaburi

Umepakiwa na: Pascal Mussa

Umepakuliwa mara 652 | Umetazamwa mara 2,121

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Ee Bwana E Bwana, E Bwana uwe pamoja nami, uwe pamoja nami Bwana, katika taabu zangu zote. 1.Aketiye mahali pa siri pake Aliye juu, atakaa katika uvuli wake Mwenyezi, nitasema Bwana ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini. 2.Mabaya hayatakupata wewe, wala tauni haitaikaribia hema yako, kwa kuwa atakuagiza malaika zake, wakulinde katika nia zako. 3.Mikononi mwao watakuchukua usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe, utawakanyaga simba na nyoka, Mwana simba na joka utawaseta kwa miguu. 4.Kwa kuwa amekaza kunipenda nitamwokoa na kumweka palipo juu, kwa kuwa amenijua jina langu, ataniita nami nitamwitikia, nitakuwa pamoja naye taabuni, nitamwokoa na kumtukuza.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa