Maneno ya wimbo
Kiitikio :
{Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu} x 4
1. Bwana ni nuru yangu na wokovu wangu, nimwogope nani.
Bwana ni ngome yangu na uzima wangu, nimhofu nani.
2. Neno moja nimelitaka kwa Bwana, nalo ndilo nitakalolitafuta,
Nikae nyumbani mwa Bwana, siku zote za maisha yangu,
Niutazame uzuri wa Bwana na kutafakari hekaluni mwake.
3. Naamini ya kuwa nitauona, wema wa Bwana wema nitauona,
Katika nchi ya walio hai, umngoje Bwana uwe hodari,
Upige moyo konde naam umngoje Bwana.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu