Mtunzi: Dr. Charles N. Kasuka
> Mfahamu Zaidi Dr. Charles N. Kasuka
> Tazama Nyimbo nyingine za Dr. Charles N. Kasuka
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Mika Wihuba
Umepakuliwa mara 252 | Umetazamwa mara 1,175
Download Nota Download MidiBwana alikuwa tegemeo langu, tegemeo langu, akanitoa akanipeleka panapo nafasi x2 Akaniponya, kwa kuwa Bwana, alikuwa kapendezwa nami, Alikuwa amependezwa nami x2.
1.Bwana alinitendea Sawasawa na Haki yangu, Sawasawa na Usafi wa Mikono yangu. Kwa maana nimezishika Njia za Bwana, Wala sikumuasi Mungu wangu.
2.Hukumu zake zote zilikuwa ziko mbele yangu, Wala Amri zake sikujiepusha epusha nazo. Nami nilikuwa mkamilifu mbele zake, nikajilinda na uovu wangu.
3.Kwa mtu mwenye Fadhili utakuwa mwenye Fadhili, kwa mkamilifu utajionyesha ukamilifu. Kwake ajitakaye, utajionyesha, na kwa mpotevu kuwa mkaidi.