Ingia / Jisajili

Bwana wajua yote, Wajua nakupenda

Mtunzi: Gabriel D. Ng'honoli
> Mfahamu Zaidi Gabriel D. Ng'honoli
> Tazama Nyimbo nyingine za Gabriel D. Ng'honoli

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio | Mafundisho / Tafakari | Miito | Moyo Mtakatifu wa Yesu | Shukrani | Ubatizo

Umepakiwa na: Gabriel D. Ng'honoli

Umepakuliwa mara 554 | Umetazamwa mara 1,567

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Bwana Wangu Yesu Kristo, umenipenda mimi ingawa sistahili. Upendo wako kwangu ni mkuu mno, nami nasema nashukuru. Bwana wajua yote wajua kuwa nakupenda. Nakuomba unitume na kuniongoza katika njia zako ili nibaki kuwa wako milele. 1. Upendo wangu kwako Bwana mimi haujakamilika naomba uukamilishe ndani ya moyo wangu 2. Upendo wako Bwana uyaongoze maisha yangu nikupende na kuishi katika pendo lako la kweli 3. Kama ulivyomwambia Petro chunga kondoo wangu ninakuomba nijalie niwachunge kondoo wako 4. Uniongoze nidumu katika pendo lako nikawalete kondoo wako kwenye heri na furaha

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa