Ingia / Jisajili

Bwana Ndiye Fungu

Mtunzi: Furaha Mbughi
> Mfahamu Zaidi Furaha Mbughi
> Tazama Nyimbo nyingine za Furaha Mbughi

Makundi Nyimbo: Zaburi

Umepakiwa na: Benny Weisiko

Umepakuliwa mara 1,125 | Umetazamwa mara 3,252

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo

KIITIKIO

Bwana ndiye fungu la posho langu, na la kikombe changu, wewe unaishhika kura yangu kura yangu. X2

MASHAIRI

  1. (suprano + Alto) Mungu unihifadhi maana nakukimbilia wewe, nimemwambia Bwana, ndiwe Bwana wangu, Bwana ndiye fungu la posho langu na la kikombe changu.
  2. (Tenno + Bass) Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri, Naam, mtima wangu, umenifundisha usiku, Nimemweka Bwana mbele yangu daima, kwa kuwa yuko kuumeni kwangu sitaondoshwa.
  3. (suprano + Alto) Kwa hiyo, moyo wangu unafurahi unafurahi, na utukufu wangu, unashangilia, mwili wangu utakaa kwa tumaini.
  4. (Tenno + Bass) Utanijulisha njia ya uzima, mbele za uso wako ziko furaha tele, na katika mkono wako wa kuume, mna mema mema ya milele.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa