Mtunzi: John Mwalai
> Tazama Nyimbo nyingine za John Mwalai
Makundi Nyimbo: Kristu Mfalme
Umepakiwa na: Nyamasyo Maneeno
Umepakuliwa mara 1,192 | Umetazamwa mara 3,250
Download NotaCheza mbali nami shetani nimetambua siri yako wewe
cheza mbali ondoka kwangu cheza mbali nami shetani
cheza mbali ondoka kwangu nimetambua siri yako
cheza mbali ondoka kwangu nimetambua siri yako
Ondoka nina Yesu rafiki
Ondoka nina Yesu rafiki na wokovu wangu
Ondoka kwangu nina Yesu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu
Ondoka nina Yesu rafiki ndiye mwamba wangu na wokovu wangu
1. i) Na nimetambua wewe ni mwalimu wa masengenyo hata fitina
ii) Eti unatoa vyeti kwao wale wanahitimu masomo haya
2. i) We, katika familia wajifanya mshahuri wa ndoa zetu.
ii) Na kwa nia yako mbaya unataka kuuvuruga uhusiano.
3. i) Na nikipokea rushwa, wanisifu mimi kuchangia ufisadi.
ii) Kiongozi kama mimi, nimejua kukuhifadhi ni mwisho wangu
4. i) Mimi kwa shirika langu, nimekosa kuwajibika sababu yako.
ii) Kwani we wataka nini,mambo yako nimetambua toweka kwangu
5. i) Ni kwa utafiti wangu,muhadhiri akiwa roho mtakatifu.
ii) Ujumbe wako shetani, kumbe wewe kalaaniwa toka zamani.