Maneno ya wimbo
Ee Mungu Ee Mungu uniumbie moyo safix2
Uifanye upya roho yangu, roho yangu iliyotulia ndani yangux2
1. Ee Mungu unirehemu sawaswa na fadhili zako kiasi cha wingi wa rehema zako, uyafute makosa yangu unioshe kabisa uovu wangu, unitakase dhambi zangu.
2. Ee Mungu uniumbie moyo safi, uifanye upya roho yangu iliyotulia ndani yangu, usinitenge na uso wako wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
3. Unirudishie furaha ya wokovu wako, unitegemeze kwa roho ya wepesi, nitawafundisha wakosaji njia, na wenye dhambi watarejea kwako.
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu