Ingia / Jisajili

Ee Yesu Karibu moyoni mwangu

Mtunzi: Emmanuel W. Shimbala
> Tazama Nyimbo nyingine za Emmanuel W. Shimbala

Makundi Nyimbo: Ekaristi / Komunio

Umepakiwa na: Emmanuel Shimbala

Umepakuliwa mara 371 | Umetazamwa mara 1,423

Download Nota Download Midi
Maneno ya wimbo
Ee Yesu wangu, karibu moyoni mwangu Ee bwana, utakase moyo wangu bwana ili nitakati. Ee Yesu wangu, nilishe kwa mwili wako Ee Bwana, uninyweshe kwa damu yako ili nipate uzima. Yesu mwema, (Yesu) anatuita sote tukashiriki karamu aliyotuandalia. Yesu mwema (Yesu) anatuita wote wenye myoyo safi tunaalikwa mezani. 1. Wote wenye moyo safi Bwana anatuita, Twendeni mezani kwake Bwana anatuita , kwa unyenyekevu twendeni kwa upole tujongeeni, kushiriki, karamu, takatifu. 2. Ndugu yangu jitazame ndani ya moyo wako, kama una kizuizi kinachokuzuia, kujongea kujongea karamu yake kiondoe haraka sana ili twende pamoja, tumpokee. 3. Nitakase dhambi zangu Yesu wa ekaristi, nijaze upendo wako yesu wa Ekaristi, unioshe uovu wangu nitakase kwa damu yako, nakuomba Ee Yesu, unisafishe.

Maoni - Toa Maoni

Hakuna maoni kwenye wimbo huu

Toa Maoni yako hapa