Mtunzi: Paschal Florian Mwarabu
> Tazama Nyimbo nyingine za Paschal Florian Mwarabu
Makundi Nyimbo: Mama Maria
Umepakiwa na: Yudathadei Chitopela
Umepakuliwa mara 13,274 | Umetazamwa mara 25,457
Download Nota Download Midi
P.F.MWARABU
Ewe Mama Maria, Mama yetu mwema, Mama wa Mungu
Sisi wanao leo tunakusalimu, salamu Mama.
1. Mama wa Yesu kristu, Mama yetu Maria, ututazame sisi tunaokuheshimu.
2. Ee Mama yetu mpenzi, sikia ombi letu, katika shida zetu, kwa mwanao tuombee.
3. Ee Mama mbarikiwa, Mama safi wa moyo, Mama mwenye huruma, uwe nasi daima.
4. Mama wa neema nyingi, Mama yetu Maria, tusaidie Mama, tufike juu mbinguni.