Mtunzi: Abel T. Msigwa
> Mfahamu Zaidi Abel T. Msigwa
> Tazama Nyimbo nyingine za Abel T. Msigwa
Makundi Nyimbo: Mazishi
Umepakiwa na: ABEL MSIGWA
Umepakuliwa mara 1,463 | Umetazamwa mara 3,674
Download Nota Download Midi1. a) Hapa wewe ni msafiri/ Simama na tazama,
b) Nimekufa le-o hii/ Kesho ni zamu yako.
Kiitikio
Ona vema, Ona vema nilivyokuwa humu,
Na nilivyo acha vyote mali zangu na jamaa X2
2. a) Nilitoka u-chi mimi/ Tumboni mwa mamangu,
b) Ninarudi u-chi mimi/ Tumboni mwa udongo.
3. a) Nilikuja pe-ke yangu/ Narudi peke yangu,
b) Kwaherini ndu-gu zangu/ Tutaonana tena.
4. a) Japo awe Su-l-tani/ Au awe M-fa-lme,
b) Saa yake i-kifika/ Lazima atakufa.