Maneno ya wimbo
TUNALETA VIPAJI VYETU
1.a) Baba Mungu twaja navyo vipaji, Tunaleta kwako Baba (pokea)/ Tulivyoandaa sisi wanao, Tunaleta kwako Baba.
b) Vyote mali yako twaleta kwako, Tunaleta kwako Baba(pokea)/Pokea Ba-ba uvibariki, Tunaleta kwako Baba.
KIITIKIO
Tunaleta kwako Mu-ngu wetu, Tunaleta kwako Mungu Muumba.
Tunaleta kwako vipaji vyetu, Tunaleta kwako Baba. X2
2.a) Mkate kiini cha ngano safi, Tunaleta kwako Baba (pokea)/ Na Divai tunda la mzabibu, Tunaleta kwako Baba.
b) Kwa sadaka kuu ya- agano, Tunaleta kwako Baba(pokea)/Pokea Ba-ba uvibariki, Tunaleta kwako Baba.
3.a) Mazao haya ya mashamba yetu, Tunaleta kwako Baba (pokea)/ Hata na fedha za mifuko yetu, Tunaleta kwako Baba.
b) Umetubariki tukavipata, Tunaleta kwako Baba(pokea)/ Pokea Ba-ba uvibariki, Tunaleta kwako Baba.
4. a) Nazo nafsi zetu tunazileta, Tunaleta kwako Baba (pokea)/ Raha na shida za maisha yetu, Tunaleta kwako Baba.
b) Kwako tunapata pu-mzi-ko kweli, Tunaleta kwako Baba (pokea)/ Pokea Ba-ba utubariki, Tunaleta kwako Baba.
(NB: Badala ya 'VIPAJI' yaweza kuimbwa 'SADAKA')
Nyimbo nyingine za mtunzi huyu