Mtunzi: Eng.Richard Samson
> Mfahamu Zaidi Eng.Richard Samson
> Tazama Nyimbo nyingine za Eng.Richard Samson
Makundi Nyimbo: Zaburi
Umepakiwa na: Richard Samson
Umepakuliwa mara 2 | Umetazamwa mara 5
Wimbo huu unaweza kutumika:
- Katikati Dominika ya 27 Mwaka C
KIITIKIO:
Ingekuwa heri leo msikie sauti yake! (Msifanye migumu mioyo yenu, msifanye migumu mioyo yenu, mioyo yenu msifanye migumu mioyo yenu) x2.
Mabeti:
1. Njoni tumwimbie Bwana, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu. Tuje mbele yake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
2. Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za Bwana aliyetuumba. Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi, tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake.
3. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake: Msifanye migumu mioyo yenu; Kama vile huko Meriba; Kama siku ya Masa jangwani, Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.